News

KATIBU MKUU WA UN TOURISM ATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA ARUSHA

Wajumbe kutoka Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism) wakiongozwa na Katibu Mkuu wa shirika hilo, Zurab Pololikashvili, leo Aprili 24, 2025 wamefanya ziara katika Hifadhi ya Taifa Arusha iliyopo jijini Arusha, kwa lengo la kujionea vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana ndani ya hifadhi hiyo. Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Zurab Pololikashvili pamoja na wajumbe wengine kutoka shirika la Utalii Duniani (UN Tourism) waliambatana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb), ambapo walitembelea maeneo kadhaa ya kipekee ndani ya hifadhi hiyo, ikiwemo maporomoko ya maji ya Tululusia sambamba na kuona kwa karibu aina mbalimbali za wanyamapori wanaoishi ndani ya hifadhi hiyo. Wajumbe hao walipokelewa na Naibu Kamishna wa Uhifadhi Steria Ndaga ambaye ni Mkuu wa Kanda ya Kaskazini, pamoja na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Eva Malya ambaye ni Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Arusha wakishirikiana na Maafisa na Askari kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA). Ziara hiyo inalenga kuongezeka ushirikiano kati ya Tanzania na mashirika ya kimataifa katika kukuza utalii endelevu na kuimarisha uhifadhi wa rasilimali za asili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo. Read More

Posted On: Apr 25, 2025

KAMATI YA BUNGE YA PAC YAIELEKEZA TANAPA KUENDELEA KUSIMAMIA MIRADI YA MIUNDOMBINU YA UTALII HIFADHI YA TAIFA SAADANI

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imetoa maelekezo kwa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kuendelea kusimamia miradi ya miundombinu ya utalii inayotekelezwa ndani Hifadhi ya Taifa Saadani ili kurahisisha watalii kufika kwa urahisi, kuchochea shughuli za kiutalii na kuongeza mapato ya Serikali. Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Japheti Hasunga (Mb), alitoa maelekezo hayo leo Machi 26, 2025, wakati wa ukaguzi wa miradi miwili inayotekelezwa ndani ya hifadhi hiyo ikiwemo uboreshaji wa barabara za ndani ya hifadhi na upanuzi wa uwanja wa ndege. Read More

Posted On: Mar 27, 2025

MAJALIWA AIPONGEZA TANAPA KWA MCHANGO MKUBWA KATIKA MAENDELEO YA SEKTA YA UTALII NCHINI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kasim Majaliwa (Mb) amelipongeza Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya sekta ya utalii nchini. Mhe. Majaliwa ameyasema hayo Machi 25, 2025 katika hafla fupi ya uzinduzi wa lango jipya la utalii la Ndea lililopo ndani ya Hifadhi ya Taifa Mkomazi katika Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro. Read More

Posted On: Mar 27, 2025

𝐊𝐀𝐌𝐈𝐒𝐇𝐍𝐀 𝐊𝐔𝐉𝐈: 𝐌𝐀𝐀𝐅𝐈𝐒𝐀 𝐍𝐀 𝐀𝐒𝐊𝐀𝐑𝐈 𝐖𝐀 𝐇𝐈𝐅𝐀𝐃𝐇𝐈 𝐘𝐀 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐁𝐔𝐑𝐈𝐆𝐈 - 𝐂𝐇𝐀𝐓𝐎 𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐄𝐍𝐈 𝐊𝐔𝐈𝐌𝐀𝐑𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐒𝐇𝐔𝐆𝐇𝐔𝐋𝐈 𝐙𝐀 𝐔𝐇𝐈𝐅𝐀𝐃𝐇𝐈 𝐍𝐀 𝐔𝐓𝐀𝐋𝐈𝐈

​Kamishna wa Uhifadhi Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Musa Nassoro Kuji, amehimiza maafisa na askari wa Hifadhi ya Taifa Burigi - Chato kuwajibika kikamilifu katika kuboresha na kuimarisha shughuli za uhifadhi na utalii. Read More

Posted On: Mar 16, 2025

​KAMISHNA KUJI AHIMIZA UADILIFU NA USHIRIKIANO KATIKA KUIMARISHA UHIFADHI KISIWA CHA RUBONDO

Kamishna wa Uhifadhi - TANAPA Musa Kuji amewataka Maafisa na Askari wa Uhifadhi katika Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Rubondo kufanya kazi kwa uadilifu, weledi, bidii, nidhamu pamoja na ushirikiano ili kutimiza adhima na malengo ya kuimarisha shughuli za uhifadhi katika Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Rubondo. Kamishna Kuji aliyasema hayo jana Machi 15, 2025 alipofanya ziara ya kikazi ya kukagua shughuli mbalimba na kufanya kikao na Maafisa na Askari hao katika ofisi za Makao Makuu ya hifadhi hiyo yaliyopo eneo la Kageye ndani ya Hifadhi hiyo iliyopo katika Mkoa wa Geita. Read More

Posted On: Mar 16, 2025

UJENZI DARAJA LA MTO KOGATENDE: SULUHU YA KUDUMU KWA UTALII NA UHIFADHI ENDELEVU SERENGETI

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Jenerali (Mst.) George Marwa Waitara ameiagiza Menejimenti ya TANAPA kuhakikisha kuwa ujenzi wa daraja la Mto Kogatende unakamilika kwa wakati na kwa ubora ili kuruhusu shughuli za uhifadhi na utalii kuendelea. Read More

Posted On: Mar 14, 2025