TAARIFA KWA UMMA
Posted On: Jan 08, 2025
Shirika la hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) linautaarifu Umma kuwa barabara kutoka Bagamoyo kupitia eneo la Makurunge hadi lango la Gama katika Hifadhi ya Taifa Saadani (yenye urefu wa kilometa 35), kwa sasa inapitika vizuri hadi hifadhini.
Awali, barabara hiyo ilikuwa haipitiki kutokana na baadhi ya maeneo ya barabara hiyo kuharibiwa na mvua zilizonyesha na kuleta changamoto kwa watumiaji wa barabara hiyo.