KAMPENI YA VOTE NOW ILIWAFIKISHA RAMADHANI BROTHERS JUU YA KILELE CHA MLIMA KILIMANJRO

Posted On: May, 11 2024
News Images

Ramadhan Brothers, vijana wataalam wa sarakasi za “head to head balance” maarufu kama “Ngata” na washindi wa tuzo za America’s Got Talent 2024 walifanikiwa kufika juu ya kilele cha Uhuru mita 5985 kutoka usawa wa bahari, ambacho ndio kilele kirefu zaidi barani Afrika kilichopo juu ya Mlima Kilimanjaro tarehe 03.04.2024.

Vijana hao waliamua kupanda mlima kupitia njia ya Marangu safari ambayo iliandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa kushirikiana na kampuni ya Utalii ya Zara Advanture.

Ramadhan Brothers walipanda mlima wakiwa na dhima zifuatazo-:

1. Kuhamasisha Utalii, kwa kumuunga mkono Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi alizozifanya katika kuitangaza Tanzania kimataifa.

2. Kuhamasisha kampeni ya TANAPA inayoitwa #VOTENOW maalum kwa ajili ya kuzipigia kura Hifadhi za Taifa Serengeti na Mlima Kilimanjaro katika kuwania tuzo za World Travel Awards, ambapo Serengeti imetajwa katika kipengele cha “Africa’s Leading National Park na Mlima Kilimanjaro katika kipengele cha “Africa’s Leading Tourist Attraction 2024.

3. Kupeleka bendera ta Taifa pamoja na tuzo zao walizoshinda katika mashindano ya America’s Got Talent mwaka jana ili kuuonyesha ulimwengu kuwa vijana hawa ni watanzania na Mlima Kilimanjaro upo kwao.

Ramadhan brothers walishukuru sana Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa kuwakaribisha na kuwapongeza kwa ushindi wao walioupata Marekani na kuamua kuwapa safari ya kuvitembelea vivutio vya Utalii maarufu Tanzania kama Mlima Kilimanjaro na Serengeti ambapo baada ya kushuka Mlimani wanatarajia kwenda kutembelea Hifadhi bora Afrika “Serengeti”.