News

TANAPA YASHINDA TUZO YA KIMATAIFA YA UBORA 2025 KWA MARA YA SITA MFULULIZO
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa mara nyingine tena limeshinda tuzo ya Ubora wa Kimataifa ya mwaka 2025 – (European Award for Quality Choice Achievement 2025) katika daraja la Diamond inayotolewa na Jumuiya ya Ulaya inayojishughulisha na utafiti wa viwango vya ubora – (European Society for Quality Research ESQR). Read More
Posted On: May 31, 2025

WAITARA AZINDUA MRADI WA MAHEMA KWA AJILI YA MALAZI HIFADHI YA TAIFA KISIWA CHA SAANANE.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini TANAPA Jenerali (mstaafu) George Waitara, amezindua huduma ya malazi ambayo ni Mahema katika Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane iliyopo jijini Mwanza kwa ajili ya kuvutia wageni wengi kutembelea na kupata huduma ya malazi tofauti na awali. Hafla ya uzinduzi wa mradi huo wa mahema uliochagizwa na ongezeko la watalii uliosabababishwa na Filamu mbili za “The Royal Tour na Amazing Tanzania” na maoni ya wageni na wadau wa utalii umeziduliwa Mei 23, 2025 katika hifadhi hiyo iliyopo katikati ya jiji la Miamba. Read More
Posted On: May 26, 2025

KATIBU MKUU WA UN TOURISM ATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA ARUSHA
Wajumbe kutoka Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism) wakiongozwa na Katibu Mkuu wa shirika hilo, Zurab Pololikashvili, leo Aprili 24, 2025 wamefanya ziara katika Hifadhi ya Taifa Arusha iliyopo jijini Arusha, kwa lengo la kujionea vivutio mbalimbali vya utalii vinavyopatikana ndani ya hifadhi hiyo. Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Zurab Pololikashvili pamoja na wajumbe wengine kutoka shirika la Utalii Duniani (UN Tourism) waliambatana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb), ambapo walitembelea maeneo kadhaa ya kipekee ndani ya hifadhi hiyo, ikiwemo maporomoko ya maji ya Tululusia sambamba na kuona kwa karibu aina mbalimbali za wanyamapori wanaoishi ndani ya hifadhi hiyo. Wajumbe hao walipokelewa na Naibu Kamishna wa Uhifadhi Steria Ndaga ambaye ni Mkuu wa Kanda ya Kaskazini, pamoja na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Eva Malya ambaye ni Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Arusha wakishirikiana na Maafisa na Askari kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA). Ziara hiyo inalenga kuongezeka ushirikiano kati ya Tanzania na mashirika ya kimataifa katika kukuza utalii endelevu na kuimarisha uhifadhi wa rasilimali za asili kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo. Read More
Posted On: Apr 25, 2025

KAMATI YA BUNGE YA PAC YAIELEKEZA TANAPA KUENDELEA KUSIMAMIA MIRADI YA MIUNDOMBINU YA UTALII HIFADHI YA TAIFA SAADANI
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imetoa maelekezo kwa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kuendelea kusimamia miradi ya miundombinu ya utalii inayotekelezwa ndani Hifadhi ya Taifa Saadani ili kurahisisha watalii kufika kwa urahisi, kuchochea shughuli za kiutalii na kuongeza mapato ya Serikali. Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Japheti Hasunga (Mb), alitoa maelekezo hayo leo Machi 26, 2025, wakati wa ukaguzi wa miradi miwili inayotekelezwa ndani ya hifadhi hiyo ikiwemo uboreshaji wa barabara za ndani ya hifadhi na upanuzi wa uwanja wa ndege. Read More
Posted On: Mar 27, 2025

MAJALIWA AIPONGEZA TANAPA KWA MCHANGO MKUBWA KATIKA MAENDELEO YA SEKTA YA UTALII NCHINI
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kasim Majaliwa (Mb) amelipongeza Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya sekta ya utalii nchini. Mhe. Majaliwa ameyasema hayo Machi 25, 2025 katika hafla fupi ya uzinduzi wa lango jipya la utalii la Ndea lililopo ndani ya Hifadhi ya Taifa Mkomazi katika Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro. Read More
Posted On: Mar 27, 2025

𝐊𝐀𝐌𝐈𝐒𝐇𝐍𝐀 𝐊𝐔𝐉𝐈: 𝐌𝐀𝐀𝐅𝐈𝐒𝐀 𝐍𝐀 𝐀𝐒𝐊𝐀𝐑𝐈 𝐖𝐀 𝐇𝐈𝐅𝐀𝐃𝐇𝐈 𝐘𝐀 𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀 𝐁𝐔𝐑𝐈𝐆𝐈 - 𝐂𝐇𝐀𝐓𝐎 𝐄𝐍𝐃𝐄𝐋𝐄𝐄𝐍𝐈 𝐊𝐔𝐈𝐌𝐀𝐑𝐈𝐒𝐇𝐀 𝐒𝐇𝐔𝐆𝐇𝐔𝐋𝐈 𝐙𝐀 𝐔𝐇𝐈𝐅𝐀𝐃𝐇𝐈 𝐍𝐀 𝐔𝐓𝐀𝐋𝐈𝐈
Kamishna wa Uhifadhi Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Musa Nassoro Kuji, amehimiza maafisa na askari wa Hifadhi ya Taifa Burigi - Chato kuwajibika kikamilifu katika kuboresha na kuimarisha shughuli za uhifadhi na utalii. Read More
Posted On: Mar 16, 2025