LAND ROVER FESTIVAL YAWEKA REKODI HIFADHI YA TAIFA ARUSHA

Hifadhi ya Taifa Arusha imepokea Magari zaidi ya 300 chapa ya Land Rover yaliyoingia hidahini kufanya safari ya pamoja kutalii kwenye Hifadhi ya Taifa ya Arusha na kuweka rekodi ya Magari zaidi ya 300 yanayoingia kwenye hifadhi ya wanyamapori kwa wakati mmoja Tamasha la Land Rover, lililofanyika Jijini Arusha tarehe 13, Oktoba 2024.
Akizungumza wakati wa mapokezi ya watalii hao, Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Eva Malya alisema
“Leo ni siku ya kipekee kwa Hifadhi ya Taifa Arusha kupokea idadi kubwa ya magari yenye chapa moja ya Land rover kutoka katika Tamasha la Land Rover
ambapo Mhe. Rais Samia alizianzisha katika kutangaza utalii kupitia filamu ya ‘Amazing Tanzania’ na ile ya ‘Tanzania Royal tour’ ambayo sasa tunaona mwitikio wa wageni kutembelea maeneo haya umekuwa mkubwa sana”
“Kupitia watalii hawa waliokuja kwenye tamasha la Land Rover inaendelea kuitambulisha Hifadhi ya Taifa Arusha katika ramani za dunia kwa kuonyesha uzuri wa hifadhi hii pamoja na kuhamasisha wageni kutembelea hifadhi hii”
Aidha, Kamishna Malya alitoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda kwa jitihada zake kuhakikisha watalii hao wanakuja kutembelea Hifadhi ya Arusha kuchangia katika pato la Taifa na kutoa rai kwa watanzania kuendelea kutumia fursa ya ukaribu wa Hifadhi ya Taifa Arusha katika utalii wa matukio.
Kwa upande wake, Kamishna wa Msaidizi wa Uhifadhi na Maendeleo ya Biashara Jully Lyimo alibainisha kuwa zao utalii wa matukio limekuwa ukishika kasi nchini na duniani kwa ujumla ambapo tumeshuhudia mwitikio mkubwa wa watalii katika matukio kama haya.
“Nitoe rai kwa watanzania wote, klabu mbalimbali za ndani na nje ya nchi kushirikiana na TANAPA katika kuendeleza utalii huu wa matukio, tunawakaribisha sana milango iko wazi wakati wote sisi tunaamini kwa kuendeleza utalii huu tutaongeza idadi kubwa ya wageni pamoja na mapato” alisema Kamishna Lyimo.